Piracy Forces Taylor Swift To Release Her Single
Posted: Thursday, August 5, 2010 by chimwemwe in Labels: ©chimwemwe christopher. All Right Reserved
0
Record Label Ya Mwimbaji wa Country-Pop Taylor Swift Imelazimika Kuachia wimbo wa kwanza wa mwanadada huyu kutoka kwenye album yake mpya siku 12 kabla ya kuachiwa kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na kuvuja kwa wimbo huo kwenye mtandao wa rununu(Internet).
Big Machine Records wamesema MP3 ya wimbo wa "Mine" uliovuja ulikuwa wa quality ya chini na waliwataka mashabiki kusikiliza wimbo wenyewe wenye quality nzuri kupitia iTunes na Redio ya Country, Haijulikani mpaka sasa ni nani anayehusika na kuvuja kwa wimbo huo.
Wimbo ambao Taylor Swift anauelezea kama wimbo wa matumaini ambao kwa haraka ulifika namba 1 kwenye chati za iTunes upo kwenye album yake ya 3 ya mwanadada Taylor Swift inayokwenda kwa jina la "Speak Now" ambayo itazinduliwa Duniani kote tarehe 25 October baada ya album yake ya pili inayokwenda kwa jina la "Fearless" kuuza zaidi ya nakala millioni 5.95 nchini Marekani na kushikilia nafasi ya 45 katika Pop Album Chart katika wiki yake ya 90.